Search This Blog

Thursday, May 27, 2021

Kikwete ni mzima wa afya - Ridhiwani

 


Ridhiwani Kikwete,  mtoto wa rais mstaafu Jakaya Kikwete amesema baba yake ni mzima wa afya.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 27, 2021 kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Katika ujumbe wake huo,  Ridhiwani amesema, "baada ya kupokea simu na jumbe mbalimbali nimeona nitumie nafasi hii kuweka kumbukizi sawa. Mzee wetu na Mzazi wetu Dk Kikwete yupo salama wa afya nyingi sana. Hana tatizo lolote kiafya na anaendelea na majukumu yake. Taarifa za aina yeyote ni za kipuuzi na za kupuuzwa.”



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...