Search This Blog

Thursday, May 27, 2021

UN: ''Mizozo imesababisha ugumu katika kupambana na Covid-19''

 


Umoja wa Mataifa (UN) ulitangaza kuwa licha ya wito wa kukomesha mizozo wakati wa janga la corona (Covid-19), mizozo iliendelea katika sehemu tofauti za ulimwengu, ambayo ilisababisha ugumu zaidi katika juhudi za kupambana na janga hilo.

Maafisa wa UN walifanya tathmini juu ya hali ya raia katika maeneo ya mizozo kwenye mkutano wa mtandaoni ulioandaliwa na Baraza la Usalama.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu Mark Lowcock, alisema kuwa ndani ya kipindi cha Covid-19, mizozo katika maeneo kuanzia Syria hadi Yemen, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hadi Msumbiji iliendelea, na hii iliathiri vibaya juhudi za kutibu wagonjwa na kusababisha kuongezeka kesi za maambukizi ya virusi.

Akiashiria kusimamishwa kwa safari za ndege, kufungwa kwa mipaka, kuwekwa vizuizi vya kusafiri na hatua za karantini kumezuia harakati za kupeleka misaada ya kibinadamu katika maeneo ya mizozo, Lowcock alisema,

"Wakati huo huo, rushwa, vikwazo, hatua za kupambana na ugaidi na vizuizi vya kiutawala vilifanya hali iwe ngumu zaidi katika juhudi za kuendesha shughuli za kibinadamu."



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...