Search This Blog

Wednesday, May 26, 2021

Kenya kupata chango ya Corona kutoka Sudan Kusini


Kenya itapokea dozi 72,000 cha chanjo ya Covid-19 kutoka kituo cha Covax wiki hii.

Chanjo hizo zilisambazwa tena kutoka Sudan Kusini baada ya maafisa wa afya wa nchi hiyo kusema hawawezi kuzitumia kabla ya muda wake wa matumizi kumalizika.

Sudan Kusini ilipokea dozi 132,000 za chanjo ya Astra Zeneca kupitia mpango wa Covax mwishoni mwa mwezi Machi.

Waziri wa Afya wa nchi hiyo Mayen Machout, aliwaambia waandishi wa habari kwamba hawana uwezo wa kutumia chanjo hizo zote kwasababu bunge ilichukua muda kuidhinisha matumizi yake.

“Pia tuligundua kuwa baadhi ya wahudumu wa afya hawakutaka kuchanjwa na muda mwingi ulitumiwa kuwaonesha watu jinsi ya kudunga chanjo ,” Dkt Machout alisema.

Sudan Kusini itasalia na dozi 52,000 ambazo zinatarajiwa kutumiwa kabla ya tarehe 18 mwezi Julai,ambao ndio muda wake wa mwisho wa matumizi, kulingana na Shirika la habari la AFP.

Mwezi Aprili, Sudan kusini ilisema ina mpango wa kutupa dozi 60,000 za chanjo ambazo muda wake wa matumizi umemalizika walizopokea kupitia msaada wa Muungano wa Afrika.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...