Faida halisi ya kampuni ya bioteknolojia ya Ujerumani ya BioNTech, ambayo ilitengeneza chanjo ya corona (Covid-19) ilifikia euro bilioni 1 na milioni 128.1 katika robo ya kwanza baada ya mauzo ya chanjo.
BioNTech ilichapisha hasara ya upotezaji wa euro milioni 53.4 katika kipindi cha kati ya Januari-Machi cha mwaka jana.
BioNTech imetangaza takwimu zake za kifedha kwa robo ya kwanza ya mwaka 2021.
Mapato ya jumla ya kampuni yaliongezeka kwa asilimia 7,138 katika robo ya kwanza ikilinganishwa na robo ile ile ya mwaka 2020, na kufikia bilioni 2 na milioni 50.
Matarajio katika masoko yalikuwa ni euro bilioni 1.71.
Kampuni hiyo ilikuwa na mapato ya euro milioni 27.7 katika robo ya kwanza mwaka jana.
Mapato ya kampuni kwa kila hisa pia yalifikia euro 4.39.
BioNTech pia ilisema kuwa pamoja na mshirika mwenzake Pfizer katika utengenezaji wa chanjo, walifanya makubaliano na nchi 91 kwa usambazaji wa dozi bilioni 1 na milioni 800 na kwamba wamekamilisha utoaji wa dozi milioni 450 za chanjo ya Covid-19 kwa nchi 91 hadi kufikia Mei 6.
BioNTech inatarajia uwezo wa uzalishaji wa chanjo kufikia dozi bilioni 3 mwaka huu na euro bilioni 12.4 katika mauzo ya dozi bilioni 1 na milioni 800 za chanjo.

No comments:
Post a Comment