Kanali Goïta aliambiwa aendeshe uchaguzi mwezi Februari mwaka ujaoImage caption: Kanali Goïta aliambiwa aendeshe uchaguzi mwezi Februari mwaka ujao
Jumuiya ya Africa Magharibi Ecowas wameiondoa Mali katika uanachama wa Jumuiya hiyo kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini humo wiki iliyopita -yakiwa ni ya pili katika kipindi cha miezi tisa.
Kiongozi wa mapinduzi na ambaye sasa ni Kanali Assimi Goïta, alihudhuria mkutano katika mji mkuu wa Ghana, Accra.
Waziri wa mambo ya nje wa Ghana Shirley Ayorkor Botchwey aliwambia waandishi wa habari kwamba jumuiya hiyo imeitolea wito Mali kumteua Waziri Mkuu mpya raiamara moja, ili kuheshimu kipindi cha mpito cha miezi 18na kufanya uchaguzi wa rais mwezi Febriari.
Ghana ilisema utulivu wa Mali ni muhimu ili Afrika Magharibi iweze kudhibiti harakati za ugaidi katika kanda hiyo.
Kanal Goïta alinyakua mamlaka baada ya kuamuru kukamatwa kwa Rais Bah Ndaw na waziri mkuu Moctar Ouane.

No comments:
Post a Comment