Mkoa wa kaskazini mwa Msumbiji wa Cabo Delgado umekumbwa na ukosefu wa utulivu kwa muda mrefuImage caption: Mkoa wa kaskazini mwa Msumbiji wa Cabo Delgado umekumbwa na ukosefu wa utulivu kwa muda mrefu
Majeshi ya Msumbiji yamezima jaribio la mashambulizi mapyakutoka kwa wanamgambo wa Kiislamu katika mji wa kaskazini wa Palma, kwa mujibu wa Rais Filipe Nyusi.
Palma iko karibu na mradi mkubwa wa gesi unaoendeshwa na kapuni kubwa ya kawi ya Total ya Ufaransa.
Mwezi Machi, mamia ya wanamgambo walio na mafungamano na kundi la Islamic State (IS) walivamia mji huo katika shambulio lililosababisha vifo vya makumi ya watu.
Rais alisema tukio la wikendi lilihusisha jaribio la wanamgambo wakijaribu kuvamia kijiji cha Lumbi, Wilaya ya Palma. Aliongeza kuwa wanamgambo hao waliwaua wenzao watano waliojaribu kujiondoa.
Bw. Nyusi alitoa tamko hilo katika mkutano wa chama tawala cha Frelimo uliofanyika Matola, Mkoa wa Maputo.
Alisema serikali yake iki tayari kuunga mkono msaada wa kigeni kukabiliana na wanamgambo kaskazini mwa nchi hiyo "hakuna mtu anayepaswa kujiona ana kinga au anaweza kupambana na ugaidi peke yake".

No comments:
Post a Comment