Mwanasiasa anayependelea sera za kizalendo nchini Israel Naftali Bennet amesema jana kuwa atajiunga na juhudi za kuunda serikali ya muungano itakayomuondoa madarakani waziri mkuu Benjamin Netanyahu.
Akizungumza baada ya kukutana na wajumbe wa chama chake cha Yamina, Bennet amesema atafanya kila linalowezekana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na kiongozi wa upinzani nchini humo Yair Lapid.
Lapid ana muda wa hadi Jumatano inayokuja kufanikisha uundaji wa muungano wa vyama utakaokuwa na wingi wa viti bungeni kumwezesha kuunda serikali mpya.
Wabunge wa Israel wanaompinga waziri mkuu Netanyahu na chama chake cha Likud wamekuwa kwenye majadiliano mazito ya kuunda muungano baada ya uchaguzi wa mwezi Machi kushindwa kutoa mshindi wa moja kwa moja wa kuunda serikali.

No comments:
Post a Comment