Search This Blog

Saturday, May 8, 2021

Iran yatoa mwito kwa UN kulaani machafuko ya Jerusalem

 


Iran imeitolea mwito Umoja wa Mataifa na taasisi nyengine za kimataifa kulaani vitendo vya polisi wa Israel katika maeneo ya msikiti wa Al Aqsa katika eneo lililotwaliwa la Jerusalem ikisema vinaweza kuhesabiwa kuwa ´uhalifu wa kivita.´ 

Msemaji wa Wizara ya kigeni Saeed Khatib-zadeh amesema Iran inalaani mashambulizi hayo huku akisema uhalifu huo wa kivita kwa mara nyengine tena unaionesha dunia namna serikali ya kiyahudi inavyotekeleza uhalifu dhidi ya watu wa palestina. 

Mvutano mjini Jerusalem umeongezeka katika wiki za hivi karibuni kufuatia maandamano ya wapalestina wakilalamikia hatua ya Israel kuwazuia kufika kwenye sehemu ya mji huo mkongwe wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, na pia kitisho cha kuziondoa familia nne za kipalestina ambao makaazi yao yanadaiwa kutaka kupewa walowezi wa kiyahudi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...