Maelfu ya watu ambao wamekuwa wakiandaa maandamano dhidi ya serikali tangu Aprili 28, waliandamana katika miji muhimu ya nchi ya Colombia.
Wawakilishi wa Muungano, vikundi vya wanafunzi na watu kutoka matabaka mbalimbali walipinga vitendo vya serikali ya Rais Ivan Duque, kufuatia wito uliotolewa na Kamati ya Mgomo wa Kitaifa.
Wanaharakati hao ambao walifunga barabara katika mji mkuu wa Bogota na Medellin ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini, walitembea barabarani na kufanya maandamano ya amani yaliyoambatana na muziki na nyimbo.
Katika mji wa Tulua huko Valle del Cauca, ambapo matukio ya vurugu yametokea tangu maandamano yalipoanza, kulikuwa na ghasia kati ya waandamanaji na polisi usiku.
Uharibifu mkubwa wa vifaa ulitokea baada ya waandamanaji kuchoma moto jengo la mahakama jijini.
Polisi waliingilia kati na kukabiliana na waandamanaji kwa kutumia mabomu ya machozi na marungu ili kuhakikisha udhibiti wa usalama katika eneo hilo.

No comments:
Post a Comment