Search This Blog

Tuesday, May 25, 2021

Congo volcano: Mamia ya watoto waliopotea waokolewa


Watoto wengi walitenganishwa na wazazi wao walipokuwa wakikimbilia usalama waoImage caption: Watoto wengi walitenganishwa na wazazi wao walipokuwa wakikimbilia usalama wao

Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, Unicef, linasema limewaokoa watoto 530 waliopotea baada ya kutenganishwa na wazazi wao walipokuwa wakitoroka mlipuko wa Volkano usiku wa JumamosiMashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Karibu nyumba 500 ziliharibiwa baada ya Mlima Nyiragongo, ambao uko sehemu ya Kaskazini mwa mji wa Goma, kulipuka.

"Tulifanikiwa kuwapata karibu watoto 530 ambao walitenganishwa na wazazi wao na kufikia sasa tumewakutanisha 360 na wazazi wao," Afisa wa nyanjani wa Unicef mjini Goma Jean Metenier aliiambia BBC.

Amesema kulikuwa na hali ya wasiwasi mlipuko ulipotokea usiku wa Jumamosi na karibu watu 25,000 walilazimika kuondoka maeneo yaliyoathirika zaidi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...