Nahodha wa boti ameripotiwa kujeruhiwa wakati vikosi vya Walinzi wa Pwani ya Libya walipowafyatulia risasi wavuvi wa Italia ambao walikamatwa katika pwani ya Libya.
Kulingana na ripoti ya shirika la habari la Italia la Rainews24, vikosi vya Walinzi wa Pwani ya Libya vilifyatulia risasi boti tatu za uvuvi zilizosajiliwa katika mji wa Sicilia wa Mazara del Vallo wakati walipokuwa wakivua samaki umbali wa kilomita 75 kutoka mji mkuu wa Tripoli, kaskazini mashariki mwa Libya.
Ilielezwa kuwa nahodha wa boti ya uvuvi ya "Aliseo" anayejulikana kwa jina la Giuseppe Giacalone, alijeruhiwa mkononi mwake.
Ilisisitizwa kuwa matibabu ya kwanza kwa nahodha aliyejeruhiwa yalifanywa na wafanyikazi katika meli ya Libeccio ya jeshi la wanamaji wa Italia.
Wakati huo huo, vyama vya kisiasa vilivyowakilishwa katika bunge la Italia vilikosoa tukio hilo na kumtaka Waziri wa Mambo ya Nje Luigi Di Maio na serikali kutoa maelezo zaidi.

No comments:
Post a Comment