Idadi kubwa ya wanafunzi walitekwa nyara kwenye shambulizi la watu wenye silaha katika Chuo Kikuu cha Kibinafsi kilichoko jimbo la Kaduna nchini Nigeria.
Watu hao wenye silaha ambao bado hawajatambuliwa, walikwenda kwenye Chuo Kikuu Kibinafsi cha Green Field katika jimbo la Kaduna hapo jana usiku na kufyatua risasi.
Wanafunzi wengi walitekwa nyara wakati wa shambulizi hilo.
Kamishna wa Usalama na Maswala ya Ndani ya Jimbo la Kaduna Samuel Aruwan, alithibitisha tukio hilo, lakini hakutoa maelezo zaidi juu ya idadi ya wanafunzi waliotekwa nyara katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari vya ndani.

No comments:
Post a Comment