Search This Blog

Wednesday, April 7, 2021

Virusi vya corona: Jinsi Kremlin inavyomlinda Rais Putin dhidi ya maambukizi


Kuanzia mwanzo wa janga la corona, mamlaka nchini Urusi zimefanya kila linalowezekana kumlinda Rais Vladimir Putin kutokana na maambukizo ya ugonjwa huo. Lakini unaandaaje karantini ya mtindo wa Kremlin na kwa gharama gani?

Katika mwaka uliopita, mamia ya watu walilazimika kujitenga nchini Urusi, kabla ya kumkaribia Vladimir Putin.

Wengine walilazimika kujitenga hata ikiwa hawakutangamana moja kwa moja na rais, lakini kama tahadhari kwa sababu walikuwa wakitangamana na watu wengine ambao walikuwa wanapanga kukutana naye.

Mnamo Machi 25, 2020, Rais Putin alihutubia taifa na kutangaza kwamba Aprili 1 itaashiria mwanzo wa "wiki isiyo ya kufanya kazi," wakati coronavirus ilipoenea haraka nchini Urusi.

Wafanyikazi maalum wa ndege ya shirika la Rossiya, wanaomhudumia Rais Putin na maafisa wengine wakuu wa serikali ya Urusi, walitengwa

Baadaye, mnamo Aprili, masharti ya kutotoka nje yalianzishwa na kufungwa kwa maduka yasiyo ya mahitaji muhimu na kupigwa marufuku kwa mikusanyiko ya watu wengi, huku watu wakianza kufanyia kazi nyumbani.

Wakati huo huo, wanachama 60 ambao ni wafanyikazi maalum wa ndege ya shirika la Rossiya, wanaomhudumia Rais Putin na maafisa wengine wakuu wa serikali ya Urusi, walitengwa kwa mara ya kwanza mnamo Machi 26, 2020 katika hoteli karibu na mji wa Moscow.

Tangu wakati huo, mamia ya marubani, madaktari, madereva na wafanyikazi wengine wanaohudumu karibu na rais na pia wageni wa rais, wamekuwa katika karantini wakijitenga katika hoteli kadhaa nchini Urusi kumlinda Rais Putin kutokana na maambukizi.

Hivi karibuni, iliripotiwa kuwa rais alipokea chanjo iliyotengenezwa nchini Urusi, ingawa haijabainishwa ni ipi, lakini mikataba na hoteli kadhaa za "karantini" inaonekana kuwa itatumika hadi mwaka ujao.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...