Mapigano yamezuka katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu kati ya makundi kinzani ya vikosi vya usalama.
Ripoti zinasema kwamba silaha kali zilitumika huku makombora yakirushwa karibu na kasri la rais.
Baadhi ya vikosi hivyo vinamuunga rais Mohammed Abdaullahi Mohammedhuku vingine vikimpinga.
Wiki iliopita bwana Mohammed anayejulikana kama Farmajo kwa utata alijiongezea muda wake ofisini.
Muhula wake uliisha rasmi mwezi Februari.
Hatua hiyo ilikosolewa naj amii ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.
Ripoti kutoka Mogadishu siku ya Jumapili zilisema kwamba kile kilichoanza kama ghasia zilisambaa hadi katika maeneo mengine ya mji ikiwemo maeneo ya kati.
Vyombo vya habari nchini humo vilisema kwamba mapigano yalikuwa kati ya vikosi vya serikali na vitengo vya usalama ambavyo vinaunga mkono upinzani.
Lakini baadhi ya wababe wa kivitana viongozi wa koo mbalimbali wanahusishwa katika ghasia hizo.

No comments:
Post a Comment