Search This Blog

Monday, April 12, 2021

TMA yatoa tahadhari ya mvua kubwa kuanzia leo


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia Aprili 12 hadi Aprili 14 katika Mikoa 15

Taarifa hiyo iliyotolewa na TMA imeonesha mvua hiyo itanyesha Aprili 12 kwenye baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani inayojumuisha Visiwa vya Pwani, Tanga, Lindi na Mtwara

Pia, mvua inatarajiwa kunyesha Aprili 13, katika Mikoa hiyo na Mikoa mingine ikiwemo Iringa, Njombe, Ruvuma, Morogoro

Aprili 14 itanyesha kwenye baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Katavi, Rukwa, Njombe, Ruvuma pamoja na Kusini mwa mkoa wa Morogoro.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...