Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger anajiandaa kujiunga na mpango wa kuinunua klabu hiyo pamoja bilionea Daniel Ek na wachezaji wake watatu wa zamani. (BeIN Sports, via Mirror)
Liverpool wangali na mipango ya kumsajili beki wa RB Leipzig's Ibrahima Konate, 21, kwa dau la pauni milioni 40 mwishoni mwa msimu, licha klabu hiyo kutangaza hasara ya pauni milioni 46 kabla ya kodi. (Mail)
Chama cha mpira wa miguu cha Ujerumani kinatarajiwa kuanza mazungumzo na kocha anayeondoka katika klabu ya Bayern Munich Hansi Flick ili kuchukua nafasi ya Joachim Low kama kocha wa timu ya taifa hilo. (90min)
Kocha wa Leicester City Brendan Rodgers hana mpango wa kuhamia Tottenham kuchukua nafasi iliyoachwa wazi baada ya kutimuliwa Jose Mourinho. (Sky Sports)
Winga wa timu ya taifa ya England Jesse Lingard, 28, atapigania kuihama klabu ya Manchester United mwishoni mwa msimu pale mkataba wake wa mkopo na West Ham utakapokatika. (Eurosport)
Inter Milan wameingia katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji Sergio Aguero, 32, ambaye ameshatangaza kuondoka Manchester City mara baada ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu. (Caciomercato - in Italian)
Mshambuliaji wa Lille raia wa Canada Jonathan David, 21, yupo katika mawindo ya Manchester United na Arsenal. (Fichajes.net - in Spanish)
Leeds United wamefanya mazungumzo juu ya kumsajili winga wa klabu ya Rubin Kazan na raia wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 20. (Football Fancast)
Tottenham wanamuwinda kiungo wa Celtic na raia wa Ivory Coast Ismaila Soro. (Mail)
Kiungo wa Brighton raia wa Uholanzi Davy Propper, 29, anawindwa na klabu yake ya zamani miamba ya soka ya Uholanzi PSV Eindhoven. (The Argus)
No comments:
Post a Comment