Search This Blog

Wednesday, April 21, 2021

Rais Biden asema hukumu ya mauaji ya Floyd haitoshi

 


Maelfu ya watu nchini Marekani, wanaendelea kushangiria hukumu ya kwanza, iliyomtia hatiani afisa polisi wa kizungu, kwa mauaji ya mtu mweusi, katika historia ya taifa hilo. 

Hata hivyo, Rais Joe Biden amesema kutiwa hatiani kwa Derek Chauvin, kwa mauaji ya George Floyd, kunaweza kuwa hatua kubwa, katika vita dhidi ya ubaguzi wa kimfumo, lakini hakutoshi. 

Biden aliyekuwa akizungumza katika Ikulu ya White House akiwa na makamu wake, Kamala Harris, muda mchache baada ya mahakama kumtia hatiani Chauvin, kwa mashitaka matatu ya mauaji, alisema Marekani haipaswi kutosheka na hukumu hiyo pekee, bali kusonga mbele hadi mfumo mzima, uwe umebadilishwa. 

Viongozi hao wawili wamelitolea wito baraza la Congress, kuyashughulikia haraka mageuzi ya polisi, ikiwemo kuidhinisha muswaada wa sheria, uliopewa jina la Floyd, aliyeuawa akiwa amegandamizwa goti shingoni, mwezi Mei mwaka jana.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...