Search This Blog

Tuesday, April 27, 2021

Naibu Waziri Kigahe kusaidia kutatua changamoto za kiwanda cha Pareto Mufindi

Naibu waziri wa viwanda na biashara Exaud kigahe amewahakikishia wamiliki wa kiwanda cha pareto kilichopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kuwa atawasaidia kutatua changamoto wanazokabiliwa nazo katika uendesheji wa kiwanda hicho ambacho kimekuwa manufaa makubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo na taifa kwa ujumla.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kiwanda hicho naibu waziri Kigahe  alisema kuwa amebaini kuwa kiwanda hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali kama kuwepo kwa biashara ya zao hilo kimagendo na kusababisha wakulima kunyonywa na walanguzi hao.

Alisema kuwa walanguzi hao wamekuwa wananua zao la pareto kwa bei ndogo huku wakitumia mizani ambayo inawanyonya wakulima hivyo amepiga marufuku kwa walangiuzi hao kuacha mara moja tabia hiyo ya kutumia mizani ambayo haijathibitishwa na wakala wa vipimo.

Kigahe aliongeza kuwa serikali itaweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha wanawadhibiti walanguzi holela wa zao la Pareto kwa kuwa wanashusha thamani ya zao hilo na kuwanyonya wakulima ambao serikali imekuwa ikipambana kuhakikisha wanaongeza thamani ya wakulima.


Alisema kuwa kiwanda cha Pareto kilichopo wilaya ya Mufindi kinauhitaji mkubwa wa zao hilo kwa kuwa hadi hivi sasa wanapata Pareto kwa asilimia 50 tu tofauti na matarajio hivyo amewaomba wakulima na wananchi wa wilaya hiyo na nyingine za mkoa wa Iringa kuchangamkia fursa ya kulima zao hilo.

Kigahe alisema kuwa kilimo cha zao la Pareto kinachukua muda wa miezi mitatu au minne kuvuna zao hilo ambao linatumia gharama nafuu na kutoa faida kubwa kwa wakuma hivyo wakulima wanahimizwa kulima kilimo cha Pareto.

 Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliamu alisema kuwa serikali ya wilaya itahakikisha kuwa walanguzi holela hawaingii katika wilaya hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wakulima wananufaika na nguvu zao wanatumia wakati wa kulima.

Alisema kuwa atakikisha anaziagiza mamlaka husika kuthibiti wanunuzi wa zao la pareto wanaotumia mizani ambayo haijathibitishwa na mamlaka ya udhibiti ubora.

Wiliam aliwaomba wananchi wa wilaya hiyo kulima zao la Pareto kwa wingi kwa kuwa linafaida kubwa katika kukuza uchumi wa mkulima na kuleta maendeleo ya nchi.

Naye mhasibu wa kiwanda hicho Gerald alimweleza naibu waziri na mkuu wa wilaya kuwa kiwanda hicho kinakabiliwa wa ufinyu wa kupata mali ghafi za kiwanda hicho hivyo anaomba serikali kutoa elimu kwa wananchi wa wilaya hiyo na mkoa wa Iringa kwa ujumla kulima zao la Pareto kwa wingi.

Alisema kuwa hadi hivi sasa kiwanda kinafanya kazi kwa asilimia 50 tu kutokana na kukosekana kwa malighafi za kutosha kuendesha kiwanda hicho.

Alimalizia kwa kuomba naibu waziri kuwadhibiti walanguzi holela ambao wamekuwa wakiwanyonya wakulima kwa kutumia mizani ambayo haijakidhi vigezo vya mamlaka husika.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...