Mvua ya wastani wa chini ina maanisha kuwa Wasomali wengi hawatakuwa na chakula cha kutoshaImage caption: Mvua ya wastani wa chini ina maanisha kuwa Wasomali wengi hawatakuwa na chakula cha kutosha
Shirika la kimataifa la misaada ya kibinaadamu linasema wimbi la makundi ya nzige, hali mbaya ya hewa na kiwango cha chini cha mvua vinamaanisha kuwa mamilioni ya watu nchini Somalia hawatakuwa na chakula cha kutosha.
Shirika la Save the Children linasema, mimea na mazao ya mboga mboga yanatarajiwa kupungua kwa 80% katika msimu huu.
Mapato yatokanayo na mauazo ya mifugo, ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Somalia, yanatarajiwa kushuka kwa hadi 55%.
Shirikka hilo linasema kuwa wanawake wanahangaika kujaribu kupata mlo mmoja tu kwa siku kwa ajili ya watoto wao. Baadhi ya watoto hao wana utapiamlo tayari.
Inakadiriwa kuwa mwaka huu, familia masikini nchini Somalia zitaweza kupata 15% ya chakula chake kutokana na mazao yao. Katika nyakati nyingine ngumu, mazao yao yamekuwa yakiwapatia karibu nusu ya chakula chao.
Wasomali tayari wanakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na ghasia za muda mrefu za wanamgambo wa kiislamu, hali tete ya kisiasa na miaka 30 ya kutokuwa na serikali kuu yenye ufanisi.

No comments:
Post a Comment