Japan imeidhinisha mpango wa kuachilia zaidi ya tani milioni moja za maji mahafu kutoka katika kiwanda kilichoharibiwa cha nyuklia cha Fukushima yaingie ndani ya bahari.
Maji hayo yatawekewa dawa ya kuyasafisha ili viwango vya mionzi viwe chini chini ya vile vya maji ya kunywa.
Lakini sekta ya wavuvi wa eneo hilo inapinga vikali hatua hiyo, sawa na Uchina na Korea Kusini.
Tokyo inasema kazi ya kuyachilia maji hayo yaliyokuwa yakitumiwa kupoza mafuta ya nyuklia itaanza katika kipindi cha takriban miaka miwili.
Kuidhinishwa kwa mara ya mwisho kunakuja bada ya miaka ya mjadala na unatarajiwa kuchukua miongo kumaliza.
Kiwanda cha nyuklia cha Fukushima kilipigwa na tetemeko la ardhi na tsunami mbaya ambavyo viliharibu eneo hilo na kufurika kemikali.
Kwasasa, maji ya mionzi yamesafishwa kupitia katika mchakato wa kuyachuja ili kuondoa kemikali za mionzi b, ikiwa ni pamoja na tritium - inayojulikana kama yenye madhara kwa binadamu tu pale inapowekwa kwa kiwango kikubwa.
Baadaye hutunzwa katika matanki, lakini waangalizi wa kiwanda cha Tokyo Electric Power Co (TepCo) wanasema wanaishiwa na nafasi, kwani , matanki hayo yanatarajiwa kujaa ifikapo mwaka 2022.
Takriban tani milioni 1.3 za maji ya mionzi - au yanayoweza kujaza madimbwi 500 ya Olyimpikya kuogelea - kwa sasa yametunzwa katika matanki haya, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la habari la Reuters.
Makundi ya mazingira kama gile Greenpeace vimekuwa vikielezea upinzani wao kwa muda mrefu dhidi ya kuachiliwa kwa maji hayo ndani ya bahari.
Shirika hilo lisilo la kiserikali (NGO) lilisema kuwa mpango wa Japan wa kuachilia maji hayo unaonesha kuwa serikali "kwa mara nyingine imewakosea watu wa Fukushima".
Sekta ya nchi hiyo ya uvuvi pia imepinga uamuzi huo, ikihofia kwamba walaji watakataa kununua samaki waliovuliwa kutoka eneo hilo.
Sekta hiyo iliathiriwa pakubwa baada ya mkasa wa mwaka 2011, huku nchi nyingi zikipiga marufuku uagizwaji wa bidhaa za baharini kutoka kwenye mwambao wa kaskazini-mashariki mwa Japan.
Uamuzi huo umekosolewa na majirani wa Japan. Kabla ya uamuzi huo, Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kusini Jumatatu ikielezea "kusikitika sana ".
Msemaji wa wizara mmbo ya nje ya Uchina Zhao Lijian pia aliitaka Japan "iwajibike ".
"kulinda usalama wa maslahi ya kimataifa ya umma na afya ya Watu wa China na usalama, Uchina imeelezea masikitiko yake kwa Japan kupitia mifumo ya Kidemokrasia ,"Bw Zhao alisema.
Marekani inaonekana kuunga mkono uamuzi wa Japan, hatahivyo, inaonekana kuwa na "kuidhinisha hayo kulingana na viwango vilivyokubalika vya kimataifa vya usalama wa nyuklia ".

No comments:
Post a Comment