Search This Blog

Sunday, April 25, 2021

Azam na Yanga pambano la kibabe leo


 REKODI zinaonesha kwamba, Oktoba 15, 2008, ilikuwa mara ya kwanza Yanga kukutana na Azam kwenye Ligi Kuu Bara ambapo matokeo ya mchezo huo, Yanga iliikaribisha vizuri Azam kwenye michuano hiyo kwa kuichapa mabao 3-1.

Huo ndiyo ulikuwa msimu wa kwanza kwa Azam kucheza Ligi Kuu Bara. Leo Jumapili, timu hizo zinakutana tena Uwanja wa Mkapa, Dar, ukiwa ni mchezo wa 26 ndani ya ligi hiyo.

Safari hii ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi vijana wanasema leo kitaumana kutokana na nafasi za timu hizo kuelekea mechi za mwisho za kumalizia msimu huu wa 2020/21.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar, Yanga ilishinda 1-0, mfungaji akiwa Deus Kaseke dakika ya 48.

Wakati ule, Benchi la Ufundi la Yanga liliongozwa na Cedric Kaze raia wa Burundi, huku lile la Azam likiongozwa na Mromania, Aristica Cioaba.

 Yanga yenye pointi 57, itatakaushinda mchezo wa leo ili kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, huku Azam yenyewe ikitaka ushindi kwa namna mbili; kupunguza wigo wa pointi dhidi ya Yanga na kulipiza kisasi kutokana na kupoteza mchezo wa kwanza nyumbani.

Katika mechi 25 zilizopita baina ya timu hizo kwenye Ligi Kuu Bara, Yanga imeshinda tisa, Azam nane na sare nane.


 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...