Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Zweli Mkhize ametangaza kusimamishwa kwa chanjo ya Covid-19 aina ya Johnson & Johnson ili kuchunguza chanjo hiyo na uhusiano uliopo na kuganda kwa damu.
Dk Mkhize alisema uamuzi huo ni "hatua za tahadhari."
Saa kadhaa kabla maafisa wa afya wa Marekani walisitisha utumiaji wa chanjo baada ya kugundulika kwa athari ambayo ni nadra ya damu kuganda.
Mamlakaya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) ilisema visa sita katika dozi milioni 6.8 viliripotiwa.
Johnson & Johnson walisema pia ilikuwa ikisitisha kutolewa kwa chanjo huko Ulaya.
Hatua hiyo ya Marekani inafuata visa vichache kama hivyo katika chanjo ya AstraZeneca, ambayo imesababisha ukomo wa matumizi yake.
Shirika la Afya duniani limeiambia Reuters kuwa inafuatilia hali ilivyo na inasubiri ripoti kutoka kwa wadhibiti wa Marekani na wa bara la Ulaya.
Hatahivyochanjo zimeanza kuwasili nchi za EU saa 24 tu kabla ya Johnson & Johnson kusema kuwa watasitisha kupeleka chanjo zao nchi za Ulaya.
Kwa kuwa hazijasimamiwa na EU, wataalamu watakuwa wanaifuatilia Marekani kuona ni hatua gani watachukua baada ya hapo.

No comments:
Post a Comment