Search This Blog

Wednesday, February 10, 2021

Watu 23 wafariki kwenye mashambulizi ya silaha nchini Nigeria

 


Watu 23 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya kushambuliwa na watu waliojihami kwa silaha nchini Nigeria.

Kamishna wa Usalama na Mambo ya Ndani wa Mkoa wa Kaduna, Samuel Aruwan, , alitoa maelezo na kuarifu kwamba washambuliaji wenye silaha ambao bado hawajafahamika waliendesha mashambulizi katika maeneo ya Birnin Gwari, Giwa, Chikun, Igabi na Kauru mkoani humo.

Aruwan alibainisha kuwa watu 23 walipoteza maisha na wengine wengi walijeruhiwa kwenye mashambulizi hayo.

Akifahamisha kuwa vikosi zaidi vya usalama vimetumwa mkoani humo kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi, Aruwan pia alisema kuwa uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na tukio hilo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...