Kampuni ya bioteknolojia ya Ujerumani ya BioNTech iliyoanzishwa na mwanasayansi wa Kituruki Prof. Dr. Uğur Şahin na mkewe Dr. Özlem Türeci, imeanza uzalishaji wa chanjo ya corona (Covid-19) iliyoboreshwa nchini humo.
Katika taarifa iliyotolewa na BioNTech, iliarifiwa kwamba dozi milioni 250 za chanjo zitazalishwa ndani ya nusu ya kwanza ya mwaka huu katika taasisi ya mji wa Marburg, na chanjo za kwanza zimepangwa kutolewa mapema Aprili.
BioNTech inalenga kuzalisha jumla ya dozi bilioni 2 za chanjo katika taasisi 6 za uzalishaji zilizoko nchi tofauti mwaka huu.

No comments:
Post a Comment