Search This Blog

Friday, February 26, 2021

Wanafunzi takribani 300 wa kike watekwa Nigeria


Mamia ya wanafunzi wa kike wametekwa nyara katika jimbo la Kaskazini-magharibi la Zamfara, BBC imeelezwa.

Mwalimu amesema takribani wanafunzi 300 wamechukuliwa wakati wa shambulilio la siku ya Ijumaa majira ya asubuhi.

Msemaji wa gavana wa jimbo amethibitisha kutokea kwa shambulio lakini hakutoa taarifa zaidi.

Hili ni tukio la karibuni la utekaji unaowahusisha watu wengi, unaolenga shule katika majuma ya hivi karibuni.

Watu wenye silaha huwateka wasichana wa shule kwa ajili ya kupata fedha.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...