Search This Blog

Saturday, February 6, 2021

Uturuki yaridhishwa na serikali ya mpito Libya


"Tunakaribisha uteuzi wa Rais, wajumbe wa Baraza la Kitaifa pamoja na Waziri Mkuu, kufuatia matokeo ya uchaguzi uliofanyika kwenye Mkutano wa Mazungumzo ya Siasa ya Libya (LSDF)  nchini Uswizi chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, watakaohudumu hadi uchaguzi utakapofanyika Desemba 24, 2021 nchini Libya."

Katika taarifa ambayo ilibaini matarajio ya Serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa itaundwa haraka iwezekanavyo kwa msingi wa ramani ya iliyoamuliwa na LSDF na kuanza majukumu yake, pia ilisema,

"Hatua hii ya kidemokrasia iliyochukuliwa na ndugu zetu wa Libya kwa msingi wa mazungumzo na upatanisho wa kitaifa ni fursa muhimu ya kulinda uhuru wa Libya, na uadilifu wa kuanzisha umoja wake wa kisiasa."

Taarifa hiyo pia ilisema:

"Mbinu za kijeshi ambazo zilikataliwa na Uturuki tangu mwanzo, pia hazitoruhusiwa wakati huu na jumuiya ya kimataifa inaamini kwamba hii imekuwa fursa ya kihistoria kuelekea kwenye suluhisho la kudumu la kisiasa.’’

Uturuki itaendelea kutoa msaada wake katika huduma za umma zinazohitajika na wananchi wa Libya, kuhakikisha usalama, kuhalalisha maisha ya kila siku na kuhusika katika usimamizi na ufuatiliaji wa uchaguzi uliopangwa kufanyika  mwisho wa mwaka kwa ajili ya muundo mpya wa serikali.

Kama matokeo ya upigaji kura wa wanachama wa LSDF, mamlaka ya mtendaji ya muda iliazimia kutawala Libya hadi uchaguzi uliopangwa utakapofanyika Desemba 24, 2021, ambapo Muhammed Menfi alichaguliwa kama Rais wa Baraza la Kitaifa, na Abdulhamid Dibeybe kama Waziri Mkuu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...