Search This Blog

Sunday, February 21, 2021

Umoja wa Mataifa walikosoa jeshi la Myanmar baada ya vifo vya watu wawili


Vifo vya waandamanaji wawili wanaopinga mapinduzi nchini Myanmar, leo hii vimezusha lawama mpya ya Umoja wa Mataifa dhidi ya utawala wa kijeshi. 


Tamko la umoja huo linatolewa wakati waombolezaji wanajiandaa na mazishi ya binti, ambae amekuwa alama ya kuupinga utawala wa kijeshi. 


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amelaani matumizi makubwa ya nguvu katika makabiliano yaliyotokea jana Jumamosi ambayo wahudumu wa kitengo cha dharura wanasema mtu mmoja amekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa. 


Katika siku za karibuni, mamlaka za Myanmar zimeongeza mbinu kuyakabili maandamano ya umma yanayoshinikiza kurudishwa madarakani kwa kiongozi wa kiraia aliyeondolewa madarakani Aung San Suu Kyi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...