Search This Blog

Monday, February 22, 2021

Ukungu wachelewesha utoaji wa chanjo za Ebola Guinea


Utoaji wa chanjo dhidi ya virusi vya Ebola nchini Guinea umecheleweshwa kwa sababu ya ukungu mwingi kuvuruga safari za ndege katika mji mkuu Conakry. Shirika la Afya Duniani - WHO lilikuwa limetangaza kuwa zaidi ya dozi 11,000 za chanjo aina ya Merck dhidi ya ugonjwa huo hatari zilitarajiwa kuwasili Conakry jana Jumapili. 

Ndege iliondoka Geneva mapema jana lakini ikaelekea Dakar, Senegal, kwa mujibu wa mkuu wa shirika la afya la Guinea Sakoba Keita, ambaye alisema itajaribu kutua Conakry leo, kama mazingira yataruhusu.

 Mji mkuu wa Guinea umefunikwa na ukungu kwa siku tatu zilizopita kwa sababu ya upepo mkali unaobeba vumbi kutoka Jangwa la Sahara, hatua ambayo imesababisha kufutwa kwa safari zote za ndege za kuingia na kutoka mjini humo hadi wakati usiojulikana.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...