Search This Blog

Friday, February 12, 2021

Tetesi za soka kimataifa

 


Nafasi ya kocha Jose Mourinho wa Tottenham Hotspur ni salama licha ya matokeo mabaya na tetesi za mashaka kutoka kwa wachezaji wakubwa. (Mirror)

Milan na Juventus wanamfuatilia winga wa Chelsea Hakim Ziyech, 27. (Calciomercato)

Leeds United, Southampton na West Ham United wanaweza kuchuana na Tottenham kuwania saini ya kiungo wa kati wa Sampdoria raia wa Denmark Mikkel Damsgaard, 20. (Star)

Arsenal walishindwa kufanya uhamisho wa mkopo kwa kiungo wa Uhispania Riqui Puig, 21, kabla ya kumpata kiungo wa kati wa Real Madrid na Norway Martin Odegaard, 22, hadi mwisho wa msimu. (Express)

Wakala wa Ismaila Sarr amesema mazungumzo yako katika hatua za juu kwa ajili ya winga huyo, 22,raia wa Senegal kujiunga na Liverpool mwezi Septemba. (Liverpool Echo)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Zenit St Petersburg, Dejan Lovren, 31, anaamini rafiki yake wa karibu na mchezaji mwenza wa zamani wa Liverpool Mohamed Salah, atakuwa Anfield kwa miaka mingi zaidi.(Talksport)

Manchester United bado haijaamua ikiwa itaongeza itaongeza mkataba wa mwaka mmoja katika mkataba wa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 34 Jumapili, na kiungo wa Uhispania Juan Mata, 32. Mlinda mlango wa Argentina Sergio Romero, 33, ambaye sasa ni chaguo la tano, ataachiliwa katika majira ya joto.(Manchester Evening News)

Mlinzi wa Uholanzi wa Bayer Leverkusen Timothy Fosu-Mensah, 22, anakubali kwamba alilazimika kuachana na Manchester United kwa sababu ya taaluma yake.(Mail)

Tottenham inatafuta jukumu muhimu kwa kiungo wa Kiingereza Oliver Skipp, 20, katika kikosi cha kwanza msimu ujao baada ya kucheza kwa mkopo Norwich City.(Football Insider)

Kiungo wa kati wa Real Madrid Luca Modric,35, amejitolea kupunguzwa mshahara ikiwa anaweza kusalia Bernabeu. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Juventus walikuwa wameazimia kumrudisha kiungo wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogba Turin mwezi Aprili 2020 na wakamtoa mmoja kati ya winga wa Brazil Douglas Costa, kiungo wa Bosnia Miralem Pjanic, mchezaji wa Wales Aaron Ramsey na kiungo wa Ufaransa Adrien Rabiot kwa kubadilishana - lakini United iliwaambia Waitaliano walitaka pauni milioni 87 kumuuza mchezaji huyo wa miaka 27. (Calciomercato)

Wakala wa Pogba Mino Raiola anasema "lazima afanye kazi kimya kimya" linapokuja suala la kiungo wa Manchester United huku kukiwa na ripoti zinazomuhusisha na kurudi Juventus. (Talksport)

Kocha wa Sutton Matt Gray anatazamiwa kujaza nafasi iliyo wazi ya Kocha wa Northampton Town. (Football Insider)

Manchester United watapaswa kuwa na subira wakati winga wa Ivory Coast Amad Diallo, 18 , akiwa anazoea kucheza England, Kocha wa kikosi cha wachezaji wa chini ya miaka 23, Neil Wood ametahadharisha. (Goal)

Mchezaji wa zamani wa nafasi ya ulinzi wa Manchester United Paul Parker amesema Kocha Ole Gunnar Solskjaer madai kuwa timu yake haiko kwenye kinyang'anyiro cha kutwaa taji ''ni kauli ya kijinga''. (Sun)

Mchezaji anayewindwa na West Ham na Leeds Matthew Bondswell, yuko kwenye mazungumzo ya kujiunga na klabu ya ligi ya primia baada ya kuondoka RB Leipzig. (Football Insider)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...