Search This Blog

Wednesday, February 3, 2021

Shinikizo la kumtimua Spika wa seneti laendelea DRC


Seneta wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo amewasilisha ombi la kufukuzwa kwa Spika wa bunge la Seneti Alexis Thambwe Mwamba.

Bw Thambwe Mwamba ni mshirika wa karibu wa rais wa zamani wa taifa hilo Joseph Kabila.

Seneta Valentin Gerengo kutoka vuguvugu la ukombozi wa DRC -Liberation of Congo, aliwasilisha ombi hilo katika ofisi ya seneti .

"Kwa mujibu wa kipegele nambari 27 cha katiba ya nchi hiyo, aya ya tano, kifungu cha 28 na aya ya 2 hadi ya 5 ya taratibu za utendaji wa seneti, tunawasilisha ombi hili ili kutaka kuondolewa kwa Spika wa Seneti ," alisema Seneta Gerengo katika barua ambayo alithibibitisha uhalali wake katika wavuti wa habari.

Seneti inafanya kikao chake cha dharura Jumatano kujadili ajenda moja tu, iliyoitwa kuchunguza na kuidhinisha kusomwa kwa mara ya pili kwa muswada wa kuidhinisha biashara huria ya bara la Afrika.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...