Search This Blog

Wednesday, February 3, 2021

Iran yaitaka Marekani kurudi katika makubaliano ya Nyuklia

Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Mohammad Jawad Zarif ameiomba Jumuiya ya Ulaya kusaidia kurudi kwa Marekani kwenye makubaliano ya nyuklia.

Akiongea na kituo cha habari cha Kimataifa cha CNN , Zarif alisema kuwa Josep Borrell, Mwakilishi Mkuu wa EU wa Mambo ya nje na Usalama, anaweza kuchukua jukumu la kusaidia makubaliano ya nyuklia yaliyotiwa saini mnamo 2015.

"Anaweza kusaidia katika uratibu wa hatua tunazohitaji kuchukua sisi na Marekani" alisema Zarif.

Zarif alibaini kuwa ikiwa Washington itachukua msimamo wa maelewano, na wao pia wangejibu kwa njia ile ile.

Rais wa Marekani Joe Biden hapo awali alisema kuwa anaunga mkono kurudi kwa makubaliano hayo, lakini kwanza, Iran lazima itekeleze majukumu yake.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...