Wafanyabiashara wawili maarufu nchini Tanzania, Harbinder Sethi na James Rugemalira wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, wakituhumiwa kujipatia fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow wana siku 1349 mahabusu sawa na miaka mitatu, miezi nane na siku nane hadi leo Jumamosi Februari 27, 2021.
Wapo mahabusu kwa kuwa wanakabiliwa na mashtaka yasiyodhaminika, huku upelelezi wa kesi yao ukiwa haujakamilika.
Seth na Rugemalira walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Juni 19, 2017 wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2027 yenye mashtaka 12.
Ukiwaona wawili hawa walivyo sasa ni tofauti na siku ya kwanza walivyofikishwa mahakamani kwa sababu kwa nyakati tofauti walikumbana na changamoto mbalimbali.
Desemba 20, 2019 aliongezeka mshatakiwa katika kesi hiyo ambaye ni aliyekuwa mwanasheria wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege na alifikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuisababishia hasara Serikali ya dola 980,000.

No comments:
Post a Comment