Search This Blog

Saturday, February 27, 2021

Nyamhanga Ataka Machinjio Vingunguti Ianze Kutumika

 


Katibu Mkuu, TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha ifikapo mwezi Machi, 2021 Machinjio ya Vingunguti iwe imeanza kufanya kazi hata kama ujenzi wake ukiwa bado haujakamilika.


Nyamhanga ametoa agizo hilo leo Jijini humo alipofanya ziara kukagua hatua iliyofikia ya ujenzi wa machinjio hayo ambapo alibaini hadi sasa 98% imefikiwa hadi kukamilika kwake.


“Kiwango cha kutoa huduma ya machinjio hii kwa kiasi kikubwa kimeshakamilika hivyo ianze kufanya kazi kwa kuchinja wanyama wachache mpaka hapo itakapokamilika kwa 100%,” amesema Nyamhanga.


Machinjio hiyo itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuchinja Ng’ombe 1,500 pamoja na Mbuzi na Kondoo 3,000 kwa siku.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...