Search This Blog

Monday, February 15, 2021

Seneta wa Garissa nchini Kenya afariki dunia


Seneta wa Garissa nchini Kenya, Mohamed Yusuf Haji(80) amefariki dunia katika hospitali ya Aga Khan, mjini Nairobi ambako alikuwa anapatiwa matibabu, kwa mujibu wa familia yake.

Haji pia alikuwa Mwenyekiti wa Jopo la kazi la Maridhiano nchini Kenya maarufu kama BBI (Building Bridges Initiative).

Haji alijiunga na utawala wa maeneo nchini Kenya mwaka 1960 kama mkuu wa wilaya na kupanda ngazi hadi kuwa miongoni mwa makamishna maarufu mikoani.

Alistaafu uongozi wa utawala wa mikoa mwaka 1998.

Mwaka 2002, aliteuliwa kuwa mbunge na mwaka 2007, akachaguliwa kama mbunge wa eneo la Ijara kwa tiketi ya chama cha Kenya African National Union (KANU).

Wakati wa kifo chake, Haji alikuwa anahudumu muhula wake wa pili kama seneta wa Garissa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...