Rais Joe Biden wa Marekani hapo jana ameliomba bunge kufanyia mageuzi sheria ya ununuzi wa silaha. Biden amesema hayo kwenye taarifa yake wakati wa kumbukumbu ya miaka mitatu tangu tukio la ufyatuaji risasi kwenye shule moja iliyoko jimboni Florida na kusababisha vifo vya watu 17.
Biden amewatolea mwito wabunge kupitisha sheria itakayowalazimu wanunuzi wa silaha kuchunguzwa kwanza historia zao pamoja na kuzuia uuzwaji wa silaha za mashambulizi na zenye uwezo wa kuchukua idadi kubwa ya risasi.
Mshambuliaji kwenye tukio hilo la Parkland Nikolas Cruz, alikuwa na bunduki aina ya AR-15 wakati aliposhambulia watu kwenye shule ya upili ya Marjory Stoneman Douglas aliyokuwa akisoma. Ingawa alikuwa akijulikana kuwa na tatizo la akili, lakini bado alifanikiwa kununua silaha kihalali.
No comments:
Post a Comment