Search This Blog

Sunday, February 7, 2021

Ramaphosa ataka mikopo nafuu kwa Afrika


Rais wa Afrika Kusini ambaye pia ni mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Umoja wa Afrika Cyril Ramaphosa amesema leo kuwa upatikanaji wa mikopo yenye masharti nafuu itakuwa jambo muhimu kuelekea ufufuaji wa uchumi wa mataifa ya Afrika ulioathiriwa na janga la COVID-19. 


Akihutubia mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika unaofanyika kwa njia ya video, Ramaphosa amesema ingawa mashirika ya kimataifa yametoa msaada mkubwa wa kifedha kupunguza athari za kiuchumi za janga la virusi vya corona, msaada zaidi bado unahitajika. 


Mzigo wa madeni unaokabili mataifa mengi ya Afrika umezidi makali baada ya kudodora shughuli za uchumi tangu kuzuka kwa janga la viruis vya corona mwishoni mwa mwaka 2019. Tangu wakati huo bara hilo lenye waakazi bilioni 1.3 limerikodi visa milioni 3.6 vya maambakuzi ya virusi vya corona na zaidi ya watu 94,000 wamekufa huku juhudi za kutoa chanjo zikifanikiwa kupata ahadi ya dozi bilioni 1.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...