Rais wa Urusi Vladimir Putin leo ameyatuhumu mataifa ya magharibi kuwa yanamtumia mkosoaji mkubwa wa serikali yake aliye kizuizini, Alexei Navalny kujaribu kuidhibiti Urusi.
Kwenye mahojiano na vyombo vya habari vya Urusi yaliyorushwa leo, Putin amesema wapinzani wa nchi hiyo wamekuwa wakiwatumia au kuwategemea wanasiasa wenye shauku ya kupata madaraka kuihujumu Urusi.
Putin pia amesema wimbi la maandamano lililoigubika Urusi hivi karibuni kupingwa kukamatwa na kufungwa kwa Navalny limechochewa na mataifa ya kigeni.
Amesema mafanikio ya Urusi kwenye masuala ya kijeshi pamoja na jinsi ilivyoshughulikia janga la virusi vya corona ikiwemo utengenezaji chanjo ya Sputnik V yameanza kuwaudhi mahasimu wa serikali mjini Moscow.
Navalny, mkosoaji mkubwa wa Putin na serikali yake alikamatwa mwezi uliopita wakati akirejea Urusi kutoka Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kisa cha kupewa sumu mwaka uliopita.

No comments:
Post a Comment