Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Jan Kubis amekutana na jenerali muasi Khalifa Haftar kama sehemu ya juhudi za kuyaunganisha makundi yanayopingana katika taifa linalokumbwa na vita la Kaskazini mwa Afrika.
Ziara yake hiyo ni kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mnamo Desemba 24. Kwenye mkutano wao katika mji wa mashariki wa Benghazi, mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa na jenerali muasi, Khalifa Hifter, walikubaliana juu ya umuhimu wa vyama vyote vya nchini Libya kujitolea ili kufanikisha uchaguzi huo unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Ziara ya Kubis ni muendelezo wa mazungumzo ya mapema mwezi huu yaliyofanyika nchini Uswisi chini ya Umoja wa Mataifa ambapo wajumbe wa Libya waliichagua serikali ya mpito, waziri mkuu na jopo la wawakilishi watatu wa baraza la rais, watakao iongoza Libya mpaka utakapo fanyika uchaguzi.
No comments:
Post a Comment