Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya hapo kesho wanatarajiwa kukutana na wasaidizi wawili wa kiongozi wa upinzani wa Urusi aliyefungwa jela Alexei Navalny.
Mkutano huo wa mjini Brussels utakaohudhuriwa na zaidi ya mawaziri 12 utafanyika kabla ya mazungumzo ya Jumatatu ijayo ambapo mawaziri wote wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya watashiriki kujadili uwezekano wa kutangaza vikwazo dhidi ya Urusi.
Taarifa za mkutano huo zimethibitishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Lithuania, Gabrielius Landsbergis ambaye amesema wanahitaji kwanza kufahamu hali halisi inayowakabili wapinzani wa serikali ya Urusi.
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borell amesema jumuiya hiyo tayari inatafakari vikwazo vipya dhidi ya Urusi kujibu matendo ya serikali ya Urusi ikiwemo ukandamizaji wa upinzani. Hata hivyo, mataifa ya umoja huo bado yamegawanyika kuhusu hatua sahihi za kuchukua dhidi ya Urusi.
No comments:
Post a Comment