Search This Blog

Tuesday, February 16, 2021

Mji wa Babati Ulio Barabara kuu ya Afrika ni tija kwa wawekezaji


Na John Walter-Babati

Halmashauri ya mji wa Babati iliyopo mkoani Manyara, katika mpango wa bajeti yake ya mwaka 2021\2022 imedhamiria kuendelea kuwavutia wawekezaji kuwekeza kwenye miradi mbalimbali  kwa lengo la kuongeza mapato ya Halmashuri.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo,  mchumi wa Halmashauri  Hamisi Katimba, amezitaja baadhi ya fursa hizo ni pamoja na Mashamba ya HANADECO Maisaka na Singu.

Mji wa Babati upo kwenye barabara kuu ya Afrika inayotoka Cairo Misri (The Great North Road or Pan-Africa Highway) hadi Cape Town Afrika ya Kusini huku ukiwa ndo mji pekee uliopo karibu na makao makuu ya nchi, Jiji la Dodoma.

Pamoja na fursa hizo, Mji wa Babati una jiografia ya hewa nzuri ya ubaridi kiasi pamoja na ziwa Babati lenye Viboko wapole.

Bajeti hiyo ni ya kwanza ya kipindi cha mpito ambacho halmashauri imejiwekea lengo la kujitayarisha kufuzu kupanda hadhi ya kuwa manispaa ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo.

Aidha ili kutimiza azma hiyo, halmashauri inatarajia kujikita katika kutangaza fursa za uwekezaji zilipo na kuimarisha miji ya pembezoni "Satellite towns" ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kwa lengo la kuongeza mapato na kutoa huduma stahiki kwa wananchi wake inaowahudumia.

Katika hatua nyingine madiwani wa Halmashauri ya mji wa Babati wamekubaliana kwa mwaka 2021/2022 kukusanya, kupokea na kutumia jumla ya shilingi Bilioni 22,066,487,914 ambazo zitatokana na vyanzo vya ndani.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Abrahamani Kololi amewataka madiwani na watendaji wa serikali kutiumiza wajibu katika majukumu yao ili wafikie malengo waliyojiwekea.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...