Search This Blog

Tuesday, February 16, 2021

Korea Kaskazini yashutumiwa kwa wizi wa data za utengenezaji wa chanjo ya corona

 


Korea Kaskazini imeshikwa ikijaribu kuiba teknolojia inayotumika kutengeneza chanjo ya virusi vya corona kutoka kwa kampuni ya utengenezaji dawa ya Marekani Pfizer, kulingana na maafisa wa kijasusi wa Korea Kusini.

Hadi kufikia sasa haijabainika ni taarifa gani hasa ambazo zimeibwa.

Shirika la kijasusi la taifa la Korea Kusini limechukua hatua binafsi na kutaarifu wabunge juu ya kinachodaiwa kuwa uvamizi, kulingana na shirika la habari la eneo la Yonhap.

BBC imewasiliana na kampuni ya Pfizer ili kupata tamko lao lakini hadi kufikia sasa bado haijasema lolote.

Korea Kaskazini bado haijawahi kuripoti hata kisa kimoja cha maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona.

Hata hivyo, nchi hiyo inatarajiwa kupokea dozi milioni 2 za chanjo ya AstraZeneca wiki chache zijazo.

Korea Kaskazini ilifunga mipaka yake mnamo mwezi Januari mwaka jana muda mfupi baada ya ugonjwa wa virusi cya corona kuanza kujitokeza nchini China.

Mnamo mwezi Novemba, kampuni ya Microsoft ilisema takriban mashirika 9 ikiwemo Pfizer zilikuwa yamelengwa na mashirika yanayoungwa mkono na serikali nchini Korea Kaskazini na Urusi.

Inasemekana makundi ya mashirika ya Korea Kaskazini kwa jina Zinc and Cerium na kundi kutoka Urusi linalojulikana kwa jina la utani Fancy Bear, yalihusika katika uvamizi huo.

Hata hivyo, Urusi ilikanusha kulenga nchi zingine katika utafiti wa chanjo.

Wakati baadhi ya uvamizi ulifeli, kampuni ya Microsoft ilionya kwamba kuna ule ambao umefanikiwa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...