Timu ya mawakili wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, imeutaja mchakato wa mashtaka dhidi ya Mrepublican huyo kama kisasi cha Wademocrat.
Mwanasheria Michael van der Veen, alisema mwanzoni mwa kuwasilisha hoja za utetezi mbele ya baraza la Seneti kwamba Trump hakuamuru vurugu katika hotuba yake aliyoitoa muda mfupi kabla ya uvamizi wa bunge Januari 6.
Waendesha mashtaka wa chama cha Democratic walikamilisha ushahidi wao dhidi ya Trump siku ya Alhamisi.
Walihoji kuwa rais huyo wa zamani anawajibika moja kwa moja kwa uvamizi wa makao ya bunge, maarufu kama Capitol, na kulisihi baraza la seneti kumtia hatiani kwa kuchochea machafuko.

No comments:
Post a Comment