Search This Blog

Saturday, February 13, 2021

Kikosi cha Namungo FC chazuiliwa uwanja wa ndege nchini Angola kwa madai wachezaji watatu na kiongozi mmoja ana corona

 


KIKOSI cha Namungo FC kimezuiliwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Luanda, nchini Angola baada ya mamlaka kudai wachezaji watatu na kiongozi mmoja wana virusi vya Corona.

Mpaka wakati wa kuandika taarifa hii timu ipo uwanja wa ndege huku utata ukitawala kutokana na mamlaka za nchi hiyo kutaka msafara mzima ama urudi Tanzania au uende karantini.

Namungo ipo Angola kwa ajili ya kuchuana na Clube Desportivo 1º de Agosto katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho, Februari 14 na kikosi kilikwea pipa jana kikiwa na msafara wa wachezaji 22 pamoja na viongozi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...