Search This Blog

Monday, February 15, 2021

Marekani kupunguza maonyesho ya ndege za F-35


Utawala wa Kikosi cha Anga cha Marekani, umeamua kupunguza ushiriki wa ndege za kivita za F-35 kwenye maonyesho ya anga kutokana na shughuli ya ukarabati wa injini zilizokuwa na hitilafu unaochukuwa muda mrefu.

Ripoti hiyo iliyotolewa na Bloomberg ilisema kwamba toleo jipya la ndege za kivita za F-35 katika mpango wa Pentagon wa dola bilioni 398, zinakabiliwa na matatizo ya upatikanaji wa injini zinazozalishwa na kampuni ya "Pratt & Whitney".

Ilielezwa kuwa utawala uliamua kuwa kutakuwa na ushiriki mdogo wa ndege za kivita za F-35 kwenye maonyesho ya anga ya mwaka 2021 na kwamba ndege za kivita za F-35 zilizo tayari kupelekwa mafunzoni kukiwa na ulazima, hazitashiriki maonyesho 8 ya anga ndani ya mwaka huu.

Afisa wa ulinzi aliyekataa kutajwa jina ambaye tathmini yake ilijumuishwa katika ripoti hiyo, alielezea shida hiyo kama "matokeo ya injini za ndege za kivita za F-35A zinazofanya kazi bila mapumziko, ambapo joto husababisha nyufa au matabaka mapema kwenye mitambo na kwa hivyo injini lazima ziondolewe na kukarabatiwa. "

Katika ripoti hiyo, ambayo ilirekodiwa kuwa kitengo cha Programu ya F-35 kiliiambia Wizara ya Ulinzi juu ya hali mbaya zaidi, ilisema kuwa asilimia 20 ya ndege za kivita zinaweza kubaki bila injini hadi 2025.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...