Search This Blog

Friday, February 12, 2021

Maeneo ya vyanzo vya Maji mto Pangani yamevamiwa


Mkurugenzi wa Bodi ya Bonde la Maji ya Mto Pangani, Segule Segule amesema katika ukaguzi wao wamebaini kuwapo kwa maeneo ya vyanzo vya maji ambayo yamevamiwa.

"Katika ukaguzi wetu tumebaini baadhi ya maeneo ya vyanzo vya maji vinavyosimamiwa na bodi ya bonde la maji ya mto pangani ambayo yapo ndani vyanzo vya maji yamevamiwa na wananchi na tayari  shughuli mbalimbali likiwemo kilimo, ufugaji na uvuvi haramu umekuwa ukifanywa," amesema Segule.

Amesema kuwa baadhi wananchi walioko ndani mita 60 kutoka vyanzo maji tayari wameshaelimishwa na kwamba hatua mbalimbali zimekwisha chukuliwa.

"Baadhi waliingia ndani ya vyanzo hivyo kwa kutokujua na wengi wanafahamu kabisa lakini tayari tumeshawaelimisha na kuwashauri, lengo ni kuhakikisha vyanzo hivyo vinakuwa endelevu," amesema Segule.

Kwa mujibu wa Segule, vyanzo vya maji zaidi 14 katika Mikoa ya Kanda ya Kaskazini vimekaguliwa na kuwekewa alama maalumu (bikon) lengo likiwa nikudhibithi  uvamizi kwenye vyanzo  na uharibifu wa mazingira.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...