Search This Blog

Thursday, February 18, 2021

Maalim Seif kuzikwa leo Mamia wajitokeza kuupokea mwili wake

 


Mamia ya wazanzibari wanaendelea kumiminika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja vilivyopo mjini Ujunga ambapo ndipo mwili wa aliyekuwa makamo wa kwanza wa Urais Zanzibar utakapoletwa kwa ajili ya dua kabla ya kusafirishwa kijijini kwake Mtambwe, kisiwani Pemba.

Kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad kinaonekana kuleta simanzi kubwa kwa wakazi wa visiwani humo na watanzania kwa ujumla.

Kisiwani Pemba ambapo ndio alikuwa ngome yake Kuu wakati wa uhai wake, punde tu baada ya taarifa za kifo chake kuenea, baadhi ya maduka yalifungwa na shughuli nyingi za mji kusimama, hivyo kufanya mji huo kuzizima kwa masaa kadhaa.

Ratiba ya mazishi inaonyesha kuwa, baada ya mwili wa marehemu utaswaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja na hatimae kwenda kupumzishwa huko kijijini kwao Mtambwe.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...