Search This Blog

Wednesday, February 24, 2021

Kampuni ya BARRICK yatakiwa kuacha kutumia magari ya kusambaza maji


Na Timothy Itembe Mara.

Kampuni ya kuchimba madini ya dhahabu(Barrick) iliyopi Nyamongo imetakiwa kuacha tabia ya kuwasambazia maji wenyeji wa vijiji vinavyozuwazunguka badala yake wavute maji kupitia mtandao wa mabomba ili kuondoa malalamiko yaliyopo.

Akitoa kauli hiyo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mwita Mwikwabe Waitara jana alisema kuwa kuifanya hivyo kutaondoa malalamiko yaliyopo kwa jamii inayowazunguka kuwa wanatumia maji yenye sumu.

“Tumepokea malalamiko mengi nay a mda mrefu kutoka kwa wananchi wetu kuwa maji wanayotumia yana sumu kutokana na uchafuzi wa mgodi ambapo wanasema kuwa  wafanyakazi wa mgodi wao wanatumia maji safi na salama sasa niagize badala ya kuwapelekea wananchi maji kwa kutumia magari tumieni nafasi hiyo kuwavutia maji ambayo ninyi mnayatumi ahumu ili nao wafaidi na kuondoa malalamiko”alisema Waitara.

Waitara aliongeza kusema kuwa kufanya hivyo kutasaidia kujenga mahusiano mazuri na kuondoa malalamiko yaliyopo kwa jamii kuwa wafanyakazi wa mgodi wanatumia maji safi na salama huku wananchi wanaowazunguka wanatumia maji yenye sumu.

Kwa upande wa Diwani Matongo Godrey Kegoye alisema kuwa wananchi kusambaziwa maji kwa kutumia magari hawaaamini maji ya magari hayo huwenda wavutiwe maji kwa kutumia mabomba.

Diwani huyo aliongeza kusema maji yanaposambazwa kupitia magari yanaongeza mgogoro kwasababu watu wanagombania maji hayo na wengine magari yanapopita yanawakuta hawapoi kwenye maeneo hali inayosababisha wakoswe.

Mkuu wa wilaya Tarime,Mtemi Msafiri alisema kuwa serikali inaomba maji yatoke kwenye mabomba na wala sio kusambaza maji hayo kupitia magari na kufanya hivyo pesa nyingi zinatumika.

Naye Meneja wa mazingira wa mgodi wa North Mara,Frenck Nyoroma alisema kuwa maji wanayosambazia wananchi nisalama kwa sababu yanapimwa na kukaguliwa kupitia wataalamu na magari yanayosambaza nisalama.

Afisa Mazingira mkoa Mara,Nawabu Stanely Myola alisema kuwa mamlaka za serikali za mitaa zimeendelea kufuatilia maandalizi mapitio na vibali vya tathimini ya adhari kwa mazingira (TAM) kwa ajili ya uwekezaji wa ndani.

Ofisi ya mazingira inahusika katika kusimamia namkufuatilia maandalizi mapitio na vibali vya TAM zaidi ya 51 imefanyiwa (TAM) na baadhi ya miradi iliyohusika kwa kipindi cha hivi karibuni ni mradi wa ujenzi wa mfumo wa kusafirisha maji taka(Sawaragesystem)na kituo cha kutibu maji taka(waste water tereatmentplant)chini ya wizara ya maji ukisimamiawa na mamlaka ya maji Musoma (MUWASA).



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...