Search This Blog

Friday, February 5, 2021

Jeshi la Uturuki lakamilisha majaribio ya komborra la meli la Atmaca kwa mafanikio


Mkuu wa Sekta ya Ulinzi ya Urais nchini Uturuki İsmail Demir, alitoa pongezi kwa wale waliochangia katika kufanikisha kombora la kitaifa la Atmaca la kupambana na meli, ambalo lilifanyiwa majaribio hapo jana. 

İsmail Demir alichapisha ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter kuhusu majaribio ya shabaha na ulengaji wa kombora la masafa marefu la Atmaca la kupambana na meli lililotengenezwa na Roketsan huko Sinop na kusema,

 "Kombora letu la kwanza la Atmaca la kupambana na meli lilifanikiwa kulenga shabaha baada ya kurushwa kutoka kwa meli yetu ya kitaifa ya TCG Kınalıa. Ninatoa pongezi kwa kila mtu aliyechangia.

 Nalitakia mafanikio mema jeshi letu la kishujaa!" Kombora la masafa marefu la Atmaca la kupambana na meli iliyoundwa na Roketsan, lilijaribiwa jana huko Sinop. 

Shughuli ya majaribio ya kombora pia ilitazamwa na Kamanda wa Vikosi vya Wanamaji Adnan Özbal na Gavana Erol Karaömeroğlu. Kamanda Özbal alisema, "Bidhaa yetu ya kitaifa ya Atmaca itahakikisha uaminifu kwa rafiki zetu na kuogopesha maadui."




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...