Search This Blog

Tuesday, February 23, 2021

Iraq yapinga NATO kuongeza idadi ya vikosi nchini


Msemaji wa Kikosi cha Operesheni ya Pamoja ya Iraq Tahsin Hafaci, alizungumzia suala la kuongeza idadi ya vikosi vya NATO nchini Iraq.

Katika aliyotoa kwenye televisheni rasmi ya serikali, Hafaci alisema,"Takwimu za kuongeza idadi ya vikosi vya NATO sio sahihi."

Hafaci aliongezea, "Itakuwa mapema kuzungumzia suala la kuongeza idadi ya vikosi vya NATO nchini Iraq na kuwasili kwa vikosi vya nyongeza."

Mwakilishi wa Bunge wa chama cha muungano cha Iraq (Shia) Naim Ubudi, aliweka wazi katika taarifa kwenye kituo cha televisheni kwamba wanapinga kuongezeka kwa vikosi vya NATO, na kusema,

“Hatujui kuwa serikali inataka kuongeza vikosi vya NATO. Kuongeza idadi ya vikosi vya NATO ni kuongeza zaidi jukumu la vikosi vya Marekani nchini Iraq."

Mbunge wa Shia, ambaye pia alitishia kwamba vikosi vya NATO havitaweza kuingia Iraq, alisema kuwa hawatakubali suala hilo kupitia bunge.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alitoa maelezo Februari 18 na kusema,"Tumeamua kupanua wigo wa wajumbe wa NATO nchini Iraq ili kusaidia vikosi vya Iraq katika vita vyao dhidi ya ugaidi na kuzuia kurudi kwa shirika la kigaidi la DAESH. Uwakilishi wetu utaongezeka kutoka wahudumu 500 hadi elfu 4. Taasisi zetu za mafunzo zitajumuishwa kwenye idara zaidi za Iraq na mikoa ya nje ya Baghdad pia."




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...