Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran Mohammed Javad Zarif amesema Umoja wa Ulaya unaweza kuwa mpatanishi wa mzozo wa Iran na Marekani unaohusu mpango wa nyuklia.Katika mahojiano na CNN hapo jana, Zarif amesema mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, anaweza kuwa mratibu wa mchakato huo.
Ameongeza kwamba Iran itakuwa tayari kupunguza uzalishaji wa madini ya urani, ikiwa Marekani itakubali kuiondolea vikwazo ilivyoiwekea wakati wa utawala wa Donald Trump.
Aidha Rais wa Iran Hassan Rouhani ameitaka Marekani kuchukuwa hatua ya kwanza katika kusawazisha mzozo huo kama ilivyochukua hatua ya kujitoa katika makubaliano hayo yaliyotiwa saini 2015.

No comments:
Post a Comment